
MAELEZO YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025 / 2026
- ENEO CHUO KILIPO:
- Chuo cha Mbeya Polytechnic kipo Mkoa wa Mbeya katika wilaya ya Rungwe mji wa Tukuyu kata ya Ibigi, karibu na kiwanda cha chai cha Wakulima. Ukifika kituo cha mabasi cha Katumba ni mita 800 tu Kwenda chuo. Tafadhali kwa wanachuo wageni piga simu hapo juu kama umeanza safari ya kuja Tukuyu.
- TAREHE YA KURIPOTI CHUONI:
Chuo kitafunguliwa tarehe 29 ya mwezi wa 9, mwaka 2025. Kutakuwa na wiki moja ya maelekezo kwa wageni (Orientation program), wanachuo wote wanaoanza mwaka wa kwanza mnashauriwa kuhudhuria wiki hii, taarifa za chuo na kozi unayosomea zitatolewa katika wiki hii.
- USAJILI WA WANACHUO WA MWAKA WA KWANZA
Usajili wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea mwaka wa pili na wa tatu utafanyika kwa wiki moja baada ya wiki ya maelezo ya chuo, wanachuo watakao chelewa baada ya wiki mbili bila taarifa ya msingi watahesabiwa kuwa wameshindwa kuendelea na masomo.
- HOSTELI
Hosteli zipo kwa wanachuo wote, na gharama yake kwa mwaka ni shilingi 300,000/= ambapo mwanachuo atagharamiwa chumba, kitanda, godoro, umeme na maji. Chakula atajitegemea na mnaruhusiwa kujipikia.
- TARATIBU ZA UHAMIAJI KWA WANACHUO AMBAO SIO WATANZANIA
Wanachuo ambao sio watanzania wanatakiwa wakamilishe taratibu zote za kuishi Tanzania kabla hawajaingia Tanzania, hivyo watatakiwa wawe na kibali cha kuishi Tanzania kabla hawajaruhusiwa kuingia darasani
- MAHITAJI YA MWANACHUO
Mwanachuo anatakiwa awe na vitu vifutavyo:-
- Sare za Chuo
Wanachuo wote wanatakiwa kuwa na sare za chuo ambazo ni suti nyeusi kipindi wakiwa darasani
- Wanaume suruali nyeusi, shati nyeupe na koti jeusi.
- Wanawake sketi/suruali nyeusi, shati nyeupe na koti jeusi.
- Viatu vyeusi na tai nyeusi kwa jinsia zote.
- Kwa Matumizi binafsi:-
- Koti Jeupe (White coat)
- Buti za Gum (Gum boots)
- Dust coat (rangi ya dark blue)
- Scientific Calculator
- Vitabu na note books
Hivyo vyote unaweza kuja kununua ukifika chuoni kwenye maduka ya pembejeo za kilimo na stationery, bei inategemea na duka.
- Vya kuwasilisha kwenye ofisi ya Usajili
- Picha ndogo ya Utambulisho uliyopiga hivi karibuni (Passport size)
- Vyeti vya kidato cha nne na vya taaluma (kwa ambao bado hawajachukua vyeti vya sekondari namba ya mtihani (Index Namba) itatumika kama mbadala wa cheti.
ZINGATIA: Kwa wanachuo ambao hawakai hosteli au wanapanga vyumba vya mtaani gharama ya vyumba vyenye maji na umeme ni kuanzia shilingi 15,000/=, 20,000/= na 30,000/= kulingana na mazingira na wamiliki wa vyumba hivyo. Iwapo una mpango wa kupanga vyumba hivyo toa taarifa mapema ili chuo kupitia serikali ya wanachuo wakusaidie kutafuta chumba ukifika usipate usumbufu na hakuna ghraama yoyote, ni kazi ambayo serikali ya wanachuo wanaifanya kwa gharama zao.
5.0 HALI YA HEWA YA MJI WA TUKUYU.
Hali ya hewa ya mji wa Tukuyu ni ya kubadilika badilika kuna msimu wa joto kwa mwezi wa 9, wa 10, wa 11, wa 12, wa 1, wa 2, wa 3 na wa 4. Mwezi 5, wa 6, wa 7 na wa 8 ni msimu wa baridi. Pia tukuyu ni mji unaopata mvua kwa miezi mingi kuliko maeneo mengine ya mkoa wa Mbeya.
Mazingira, mji wa Tukuyu una mazingira safi na nadhifu, ni mji ambao una uoto wa kijani hivyo mazingira yanavutia kwa kuwa na nyasi za kijani na ndio chimbuko la Green city (Jiji la kijani),
Wilaya la Rungwe ina vivutio vingi vya utalii zaidi za 25 kama; ziwa Ngosi, Daraja la Mungu, ziwa Kisiba, mlima Rungwe, majengo ya zamani ya wakoloni wajerumani, maporomoko ya maji Kaporogwe na mengineyo, wanachuo wetu watapewa fursa ya kutembelea vivutio hivyo vyote vya utalii ambavyo watalii wanatoka duniani kuvifuata.
6.0 TAARIFA ZA ADA:
6.1 AWAMU ZA ULIPAJI WA ADA
Ada ya chuo unaweza kulipa yote unapoanza masomo au kwa awamu mbili au nne kulingana na uwezo wa mzazi. Mchanganuo wa ada umeoneshwa kwenye jedwari hapa chini:-
SEMISTA | MAELEZO | ADA |
SEMISTA I 495,000/= | Mwanzo wa semista ya I | 245,000/= |
Katikati ya semista ya I | 250,000/= | |
SEMISTA II 500,000/= | Mwanzo wa semista ya II | 250,000/= |
Katikati ya semista ya II | 250,000/= | |
JUMLA | 995,000/= |
6.2 GHARAMA YA MOJA KWA MOJA NA HOSTELI (DIRECT COST AND HOSTEL FEES)
Gharama za moja kwa moja zitalipwa mwanzo wa kila semista au kwa awamu mbili kama jeedwari hapa chini linavyojieleza:-
SEMISA | MAELEZO | KIWANGO | AWAMU YA 1 |
Semista I | Mafunzo kwa vitendo (Practical fee) | 100,000/= | 205,000/= |
Udhibiti Ubora NACTVET (quality assurance fee) | 15,000/= | ||
T-shirt | 20,000/= | ||
Stationery na mitihani (Stationery & Exam fee) | 50,000/= | ||
Kitambulisho cha chuo (Identity Card) | 20,000/= | ||
Semista II | Mafunzo kwa vitendo (Practical fee) | 100,000/= | AWAMU YA 2 |
Stationery na mitihani (Stationery & Exam fee) | 50,000/= | 150,000/= | |
JUMLA | 355,000/= |
6.3 MALIPO YA ADA, HOSTELI NA GHARAMA ZA MOJA KWA MOJA
Malipo yote ya Ada, Hosteli na gharama za moja kwa moja yafanyike kwenye akaunti ya benki ya chuo yenye taarifa zifuatazo:-
Taarifa za benki ya Chuo
Benki: BENKI YA BIASHARA YA TAIFA (NATIONAL BANK OF COMMERCE -NBC)
Jina la Akaunti ya Chuo: MBEYA POLYTECHNIC COLLEGE
Namba ya Akaunti: 038174033407
“MBEYA POLYTECHNIC COLLEGE- TO LEARN IS TO CHANGE”